OHOOO!! SHAMSA FORD DECIDE TO STEP IN WOLPER'S FOOT AFTER TAKING X-BOYFRIED OF WOLPER.READ HERE FOR DETAILS >>>>
HAPA CHINI▼▼


HAPA CHINI▼▼



SHAMSA AJIACHIA
Katika picha hizo ambazo Wikienda linashikilia ‘nakala’ zake, Shamsa anaonekana akijiachia na Chid Mapenzi huku akiwa amemziba sura.
Ilidaiwa kwamba, bidada huyo alidhani watu hawatamtambua jamaa huyo lakini ‘watu wabaya kwa ubuyu’ ambao wanamjua vizuri Chid Mapenzi, hawakusita kuchukua hatua kwani ndani ya dakika sifuri walitupia jina lake na picha za tatuu yake kuonesha ushahidi kuwa ni yeye.
MANENO YAIBUKA
Baada ya kutajwa kwa jina hilo ndipo yakaibuka maneno mengi ikiwa ni pamoja na kejeli za kumsema Shamsa kuwa ‘amepotea’ kwa mwanaume huyo kwani alishakuwa na uhusiano wa kupika na kupakua na Wolper.
Kama kawaida, Mwandishi wa Ubuyu alifuatilia sakata hilo hatua kwa hatua ili kubaini ukweli kama Wolper aliwahi kutoka na Chid Mapenzi.
Katika ufukunyuzi wa hali ya juu wa Wikienda, ilibainika kwamba, kuna ukweli ambao ulipatikana kupitia marafiki wa karibu wa Wolper.
UHAKIKA?
Huku akiomba hifadhi ya jina gazetini, mmoja wa marafiki hao wa Wolper alimhakikishia mwanahabari wetu kuwa hakuna shaka kwamba Wolper alishakuwa mtu wa Chid Mapenzi lakini ni kitambo kidogo.
ETI WALIPENDANA MNO!
“Ni kweli hata yeye (Wolper) hawezi kubisha kwa sababu amekuwa na Chid japokuwa ni zamani kidogo.
“Wapo wanaosema walimwagana lakini wakarudiana kisha wakaachana tena ila mimi hilo la kumwagana na kurudiana kisha kumwagana tena sina uhakika nalo lakini ukweli ni kwamba walikuwa wakipendana mno hadi wakawa kero kwa baadhi yetu,” kilinyetisha chanzo hicho.
BOFYA HAPA KUMSIKIA SHAMSA
Baada ya kuupokea kwa mikono miwili ubuyu huo, mwanahabari wetu alimtafuta Shamsa na kumuuliza sababu ya yeye kuingia kwenye penzi alilopitia Wolper ambapo intavyu ilikuwa hivi;
Wikienda: Shamsa mambo vipi? Kuna madai kwamba, mwanaume uliyenaye kwa sasa ambaye ni Chid Mapenzi aliwahi kutoka na Wolper, je, unalijua hilo?
Shamsa: Mwanaume yupi huyo?
Wikienda: Humjui? Kwani sasa hivi unatoka na mwanaume gani, si yule mfanyabiashara Chid Mapenzi?
Shamsa: Jamani mimi nashangaa watu wanasema eti sisi ni wapenzi. Jamani Chid ni patna wangu kwenye biashara.
Wikienda: Patna wa biashara? Tangu lini wewe umeanza kufanya biashara na Chid Mapenzi? Au ni filamu?
Shamsa: Hapana, nimeweka pesa zangu kwenye duka lake la nguo, tunafanya wote biashara wakati nasubiria kufungua duka langu.
Wikienda: Lakini madai ya kuwa aliwahi kuwa bwana wa Wolper unayajua?
Shamsa: Mimi na yeye hatuongei mambo hayo hivyo mimi sijui kama aliwahi kuwa na uhusiano na Wolper.
WOLPER ASAKWA
Baada ya mahojiano na Shamsa, mwandishi wetu alimwendea hewani Wolper lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo kitengo cha ubuyu kinaendelea kumsaka ili kumsikia anazungumziaje suala hilo?
NENO LA MHARIRI
Kama Wolper na Chid walikuwa wapenzi enzi hizo, hilo halimzuii Shamsa kuwa na uhusiano na mfanyabiashara huyo. Kibaya ingekuwa ni kama Shamsa angeingilia penzi hilo likiwa hai kwani tujuavyo mwanamke kama hajaolewa anaweza kuolewa na mwanaume yeyote na pale Mungu alipokupangia huwezi kupangua.
Ila nawasihi wasanii kuchunguza wanaume kabla ya kuingia nao kwenye mapenzi ili kuepusha kuhesabiwa idadi ya wanaume kwani Shamsa hajui sababu za Wolper kuachana na bwana huyo na yeye inawezekana ameingia kwa lengo la kutafuta ndoa baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Dickson Matoke ‘Dick’ aliyezaa naye mtoto wa kiume, Terry.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 comments: